
PENUELI
CHRISTIAN CENTRE – KIGOGO MBUYUNI
P
O BOX 15155 DAR-ES-SALAAM
MOB
0718-693535, 0767-693535, 0784-526464.
Email
pcctag@gmail.com
SOMO:
UBATIZO WA MAJI MENGI MARKO 16:15-16; MATHAYO 28:19;
1. Ni nini maana ya ubatizo?
Neno batiza linatokana na
neno la Kiyunani babtizo – lenye maana ya zamisha kabisa
katika maji au gharikisha. Ili mtu awe amebatizwa lazima azamishwe katika maji.
2. Je ubatizo unaondoa
dhambi?
Jibu: Ubatitizo hauondoi
dhambi, ila ni damu ya Yesu ndiyo inaondoa dhambi. Ebr 9:22; 1Yoh 1:9;
Mtu anapokea msamaha wa dhambi baada ya kutubu
dhambi zake na kumwamini Yesu kuwa BWANA na mwokozi na ndipo anabatizwa.
Tunambatiza mtu aliyeacha
dhambi si ili aache dhambi.
3. Kwa nini basi tubatizwe
kama ubatizo hauondoi dhambi?
Sababu za kubatizwa
i.
Yesu aliagiza tubatizwe
Mathayo
28:19; Marko 16:15-16;
ii.
Yesu mwenyewe
alibatizwa Mathayo 3:13-16;
iii.
Yesu mwenyewe alibatiza
Yohana
3:22; Yohana 4:1-2;
iv.
Ni tendo la
kujitamburisha na Yesu, ni mfano wa kufa na kufufuka na Yesu Rumi
6:3-5;
v.
Ni ushahidi wa nje wa
kazi iliyofanyika ndani Tito 3:5;
vi.
Ni tangazo kwa
ulimwengu wote kwamba umemvaa Kristo. Galatia 6:17;
vii.
Ni tendo utii Mathayo
3:16; Mathayo 7:24-28;
4.
Nani abatizwe? Marko 16:15-16;
a) Awe ameamini – amemkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi kwa kutubu
dhambi na kuziacha (Awe ameokoka)
b)
Lazima awe mtu mzima
kimwili na kiroho – Asiwe mtoto mdogo Marko 10:13-15; Kwa nini watoto
hawabatizwi wanawekwa wakfu?
-
Kwa sababu Mungu amewakubari,
ufalme wa Mbinguni ni wao.
5.
Ubatizo wa kweli ni upi?
Jibu: Ni wa maji mengi. Kwa nini ubatizo
wa maji mengi ni wa kweli?
a.
Ndiyo maana halisi ya neno
Batiza.
b.
Yesu alibatizwa kwa ubatizo huo
Mathayo 3:13-16;
c.
Mitume walibatiza kwa ubatizo
huo Yoh 4:1-2;
d.
Kanisa la kwanza walibatiza
hivyo Mdo 8:37-39;
6. Kanuni gani za ubatizo
sahihi?
-
Ni kwa jina la Baba, Mwana na
Roho Mtakatifu. (Utatu Mtakatifu)
-
Mathayo 28:19; Yesu mwenyewe
aliagiza hivyo.
7. Aina za ubatizo zilizopo
kwenye Biblia.
Zipo aina 7 lakini
tutaangalia muhimu 3:-
a.
Ubatizo kwa walioamini wote
(waliokoka) katika maji mengi Mathayo 28:19; Huu ndiyo ubatizo alioagiza Yesu.
b.
Ubatizo wa Yohana Mdo 19:3; Huu
ulikuwa ni ubatizo wa kuwaandaa watu wamwamini Yesu.
c.
Ubatizo wa Roho Mtakatifu Mdo
1:8; Mdo 2:1-4; Huku ni kujazwa na Roho Mtakatifu na kufunikwa na nguvu za Roho
Mtakatifu.
8. Mabatizo ya Uongo:-
Ubatizo huu upo wa aina
mbili mbili.
a.
Ubatizo wowote usio wa maji
mengi ni wa uongo.
b.
Ubatizo wa maji mengi
anaobatizwa mtu kabla ya kuokoka ni wa uongo na ni batili.
Mfano; wa mabatizo ya uongo:-
i.
Ubatizo wa maji kidogo –
Protestants wengi.
ii.
Ubatizo wa Bendera – Salvation
army
iii.
Ubatizo wa Ishara ya Msalaba
mfano ni la Apostolic n.k