Tuesday, 3 October 2017

UBATIZO WA MAJI MENGI


DSC_3455 TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD

PENUELI CHRISTIAN CENTRE – KIGOGO MBUYUNI

P O BOX 15155 DAR-ES-SALAAM

MOB 0718-693535, 0767-693535, 0784-526464.


SOMO: UBATIZO WA MAJI MENGI MARKO 16:15-16; MATHAYO 28:19;

1.       Ni nini maana ya ubatizo?

Neno batiza linatokana na neno la Kiyunani babtizo – lenye maana ya zamisha kabisa katika maji au gharikisha. Ili mtu awe amebatizwa lazima azamishwe katika maji.

2.       Je ubatizo unaondoa dhambi?

Jibu: Ubatitizo hauondoi dhambi, ila ni damu ya Yesu ndiyo inaondoa dhambi. Ebr 9:22; 1Yoh 1:9;

 Mtu anapokea msamaha wa dhambi baada ya kutubu dhambi zake na kumwamini Yesu kuwa BWANA na mwokozi na ndipo anabatizwa.

Tunambatiza mtu aliyeacha dhambi si ili aache dhambi.

3.       Kwa nini basi tubatizwe kama ubatizo hauondoi dhambi?

Sababu za kubatizwa

i.                    Yesu aliagiza tubatizwe Mathayo 28:19; Marko 16:15-16;

ii.                  Yesu mwenyewe alibatizwa Mathayo 3:13-16;

iii.                Yesu mwenyewe alibatiza Yohana 3:22; Yohana 4:1-2;

iv.                 Ni tendo la kujitamburisha na Yesu, ni mfano wa kufa na kufufuka na Yesu Rumi 6:3-5;

v.                   Ni ushahidi wa nje wa kazi iliyofanyika ndani Tito 3:5;

vi.                 Ni tangazo kwa ulimwengu wote kwamba umemvaa Kristo. Galatia 6:17;

vii.               Ni tendo utii Mathayo 3:16; Mathayo 7:24-28;

4.       Nani abatizwe? Marko 16:15-16;

a)      Awe ameamini – amemkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi kwa kutubu dhambi na kuziacha (Awe ameokoka)

b)      Lazima awe mtu mzima kimwili na kiroho – Asiwe mtoto mdogo Marko 10:13-15; Kwa nini watoto hawabatizwi wanawekwa wakfu?

-          Kwa sababu Mungu amewakubari, ufalme wa Mbinguni ni wao.

5.       Ubatizo wa kweli ni upi?

Jibu: Ni wa maji mengi. Kwa nini ubatizo wa maji mengi ni wa kweli?

a.       Ndiyo maana halisi ya neno Batiza.

b.      Yesu alibatizwa kwa ubatizo huo Mathayo 3:13-16;

c.       Mitume walibatiza kwa ubatizo huo Yoh 4:1-2;

d.      Kanisa la kwanza walibatiza hivyo Mdo 8:37-39;

6.       Kanuni gani za ubatizo sahihi?

-          Ni kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. (Utatu Mtakatifu)

-          Mathayo 28:19; Yesu mwenyewe aliagiza hivyo.

7.       Aina za ubatizo zilizopo kwenye Biblia.

Zipo aina 7 lakini tutaangalia muhimu 3:-

a.       Ubatizo kwa walioamini wote (waliokoka) katika maji mengi Mathayo 28:19; Huu ndiyo ubatizo alioagiza Yesu.

b.      Ubatizo wa Yohana Mdo 19:3; Huu ulikuwa ni ubatizo wa kuwaandaa watu wamwamini Yesu.

c.       Ubatizo wa Roho Mtakatifu Mdo 1:8; Mdo 2:1-4; Huku ni kujazwa na Roho Mtakatifu na kufunikwa na nguvu za Roho Mtakatifu.

8.       Mabatizo ya Uongo:-

Ubatizo huu upo wa aina mbili mbili.

a.       Ubatizo wowote usio wa maji mengi ni wa uongo.

b.      Ubatizo wa maji mengi anaobatizwa mtu kabla ya kuokoka ni wa uongo na ni batili.

        Mfano; wa mabatizo ya uongo:-

i.                     Ubatizo wa maji kidogo – Protestants wengi.

ii.                   Ubatizo wa Bendera – Salvation army

iii.                  Ubatizo wa Ishara ya Msalaba mfano ni la Apostolic n.k

 

1 comment:

  1. Yote mimi nimeyasoma kutoka watu mbalimbali lakini ili niweze kuelewa nina maswali machache
    1. Matumizi ya maji katika ubatizo ni nini? Kwanini tutumie maji?
    2. Ubatizo wote kabla ya Yesu ulifanyika kwenye mito (maji mengi). Ni kwanini sisi tutumie madimbwi badala ya kuwapeleka kwenye mito ambayo maji yanatiririka?
    3. Je, ni kweli hawa wanaobatizwa wakiwa watu wazima hawana dhambi?
    4. Maana za maneno na matumizi yake hutofautiana. Mswahili akisema shikamoo (salamu) mhehe lazime atumie shikamoo hiyo hiyo akisema kamwene siyo salamu? Kwani tafsiri ya ubatizo ni nini? Kwanini uzamishwe?

    ReplyDelete